Atiwa Mbaroni Kwa Kuwabaka wanawake na Kuwapiga Picha za Uchi
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Morogoro limemkamata mkazi wa mjini humo, Mabula
Mabula maarufi Six kwa tuhuma za uporaji wa simu kwa kutumia pikipiki,
kubaka na kuwapiga picha za utupu wanawake kisha kuzisambaza mitandaoni.
Akizungumza
leo Jumatatu Machi 26, 2018, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ulrich
Matei amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa baada ya makachero, kikosi cha
kupambana na uhalifu mitandaoni pamoja na kikosi cha kupambana na
ujambazi, kumfuatilia kwa ukaribu.
Akihojiwa
mara baada ya kukamatwa, Mabula ameeleza mbinu anazotumia ikiwa ni
pamoja na kujifanya askari polisi, kuwakamata wanawake nyakati za usiku,
kuwasingizia makosa mbalimbali na kuwapeleka maeneo yenye giza na
kuwabaka.
Mtuhumiwa
huyo ameyataja maeneo anayofanyia matendo hayo kuwa ni Msamvu Relini na
kwamba amekuwa akitumia mapanga kuwatisha wanawake hao na kuwapiga
picha za utupu na baadaye kutishia picha hizo kuzituma kwenye mitandao
ya kijamii.
“Hizo
picha huwa nawapiga kwa kutumia simu zao na anayekataa kunipa hela huwa
naondoka na simu yake na kisha natuma hizo picha kwenye mitandao
iliyopo kwenye simu hizo, baada ya hapo simu naiuza napata hela,”
amesema mtuhumiwa huyo.
Katika
mahojiano na polisi, mtuhumiwa huyo amemtaja mwezake mmoja Ramadhani
Salumu maarufu Miondoko mkazi wa Manispaa ya Morogoro kuwa ndio mnunuzi
wa simu hizo za wizi.
Katika msako huo polisi wamefanikiwa kumkamata Salumu na kwamba wote watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

No comments: