Alikiba Awashauri Wasanii wa Zamani Kucheza na Nyakati, Muziki Umebadilika
Msanii
wa bongo fleva nchini, Alikiba ametoa ushauri kwa wasanii wa zamani
kuwa pamoja na kwamba muziki wao ulikuwa na changamoto nyingi sana enzi
zao lakini wanatakiwa kukumbuka kuwa muziki umebadilika hivyo wanatakiwa
kuyakubali hayo.
Alikiba
anasema kuwa anajua kuwa wasanii wa zamani ndio walioufikisha muziki
huu hapa lakini wanapaswa kujua kuwa kwa sasa muziki umebadilka sana
hivyo ni lazima kukubaliana na hayo na endapo watabadilika pia
itawasaidia kwa sababu muziki wa sasa una pesa sana kuliko ule wa
zamani.
"Napenda
changamoto wanazopitia wasanii wa zamani, kwa sasa wanapaswa kujua
kuwa muziki umebadilika sana .Ukiangalia wao wameutoa muziki mbali sana
kitu ambacho sisi tunashukuru kwa sababu tumeukuta na tunauendeleza.
"Sisi
tunaona unatupatia faida kuliko wale wa zamani,zamani muziki ulikuwa
hauna ela ila siku hizi muziki una pesa japokuwa hata mimi nimeutoa
mbali hivyo hivyo.-Aliongea Alikiba alipokuwa akiongea na XXL ya Cloud
Tv.

No comments: