Header Ads

SIKU YA FIGO DUNIANI:

Wizara ya Afya imesema idadi ya wagonjwa wenye matatizo ya figo nchini imekuwa ikiongezeka ambapo utafiti uliofanyika Kanda ya Kaskazini mwaka 2014 ulionyesha kuwa kati ya asilimia 7 mpaka 15 ya Watanzania wana matatizo sugu ya figo.

Naibu Waziri wa Afya Dk. Faustine Ndugulile amesema matatizo hayo sugu ya figo kwa asilimia kubwa yamekuwa yakichangiwa na magonjwa ya shinikizo la damu na kisukari.
Amesema pia utafiti uliofanywa na Hospitali ya Kanda Bugando unaonyesha kuwa asilimia 83 ya wagonjwa wa kisukari wana matatizo sugu ya figo na kati ya hao asilimia 25 walikuwa wanahitaji huduma za usafishaji damu.
Magonjwa ya figo yanakadiriwa kuwaathiri takribani wanawake milioni 195 duniani kote na yakishika nafasi ya Nane (8) katika vyanzo vya vifo vya wanawake duniani huku ikikadiriwa kuwa wanawake takribani laki sita (6) hupoteza maisha kutokana na matatizo ya figo duniani kote kila mwaka.

No comments:

Powered by Blogger.