Header Ads

ameteketeza Jumla ya Nyavu 39 zilizokuwa zikitumika katika #Uvuvi_Haram

#Jembe_la_Watanzania
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh #Evod_Mmanda akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Ndg #Omari_Kipanga sambamba na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya,

ameteketeza Jumla ya Nyavu 39 zilizokuwa zikitumika katika #Uvuvi_Haram kutoka kwenye Kijiji cha #Namela na Kitongoji cha Ng'wale Kata ya #Msangamkuu ambapo Wananchi wa Maeneo hayo wameapa kutoendelea na Uvuvi huo haram.

Wakiongea na #Jamiifm_Radio Wananchi wa Maeneo hayo wameiomba Serikali kuendelea kutoa Elimu ya hasara itokanayo na Uvuvi haram kwenye Maeneo mbalimbali yaliyoguswa na Bahari ya Hindi.

Aidha Mh Mmanda amesema hawezi kurudi nyuma katika Swala hili na kuwataka Wananchi wote kuunga Mkono juhudi za Raisi #John_Magufuli ili kupata Maendeleo kwa kuwa Uvuvi huo unaharibu Samaki Wadogo hata matumbawe na kupunguza idadi ya Samaki baharini na hivyo kupunguza Mapato ya Nchi kupitia Bahari.

No comments:

Powered by Blogger.