Lissu afurahiswa na ujio Bombardier Q400
"Msemaji wa Ikulu, Gerson Msigwa, na kabla yake Msemaji wa Serikali, Abbas, hawajasema, hadi sasa ni kwa nini Bombardier yetu ilikuwa imezuiliwa Canada. Hawajasema kama ni kweli au la kwamba ndege yetu ilikuwa imezuiliwa kwa sababu kuvunjwa mkataba kimakosa na aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wakati huo. Nafurahi kusikia taarifa za kuachiliwa kwa ndege yetu. Nitafurahi zaidi tukiambiwa Bombardier hiyo imeachiliwa kwa masharti gani, kwa vile tulikuwa tunadaiwa karibu USD milioni 40 zilizotokana na kuvunjwa mkataba na Serikali kushindwa kesi na SCEL. Hili ni swali ambalo kila mmoja wetu anatakiwa kuwahoji hawa watoa taarifa za kuachiliwa kwa Bombardier" alisema Tundu Lissu
Baada ya jana taarifa kusambaa juu ya kuachiwa kwa ndege hiyo kuna watu walianza kudai kuwa ujio wa ndege hiyo ni pigo kwa watu ambao walikuwa sababu ya ndege hiyo kushikiliwa Canada, hivyo Tundu Lissu ametaka hao watu wafahamike kwa serikali kutoa sababu zilizopelekea ndege hiyo kushikiliwa Canada kabla ya kuachiwa jana.
"baadhi ya watu wamedai mitandaoni kwamba kuletwa kwa ndege hiyo ni pigo na aibu kwa mawakala wa mabwanyenye waliosababisha ndege yetu kushikiliwa Canada. Mimi nauliza: Hivi 'mawakala wa mabwanyenye' waliosababisha ndege yetu ikamatwe Canada ni akina nani hasa?"
No comments: