Bangi zateketezwa kwenye hifadhi
Zaidi ya ekari tatu za bangi zimeteketezwa kwenye msitu wa hifadhi ya
Maisome iliyopo katika kisiwa cha Maisome Wilayani Sengerema Mkoani
Mwanza .
Kwa
mujibu wa Katibu Tawala Wilaya ya Sengerema, Alan Mhina, bangi hiyo
ilikuwa imelimwa kwenye sehemu ya msitu huo wenye ukubwa wa hekta
12,800, na kwamba, iliteketezwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya
katika operesheni maalum ya kukomesha kilimo cha zao hilo haramu.
Kwa upande wake, Meneja Wakala wa Misitu Tanzania, TSF, Wilaya ya Sengerema, Bw. Urio Jeremiah, amesema, operesheni hiyo pia imelenga kukomesha shughuli nyingine za kibinadamu zinazotishia uhai wa hifadhi hiyo.

No comments: