Naibu Katibu Mkuu BAVICHA afunguka kujiuzulu
Naibu Katibu Mkuu wa BAVICHA, Getrude Ndibalema amefunguka na kusema
kuwa ameamua kujiuzulu nafasi yake hiyo katika chama cha CHADEMA na
kubaki mwanachama wa kawaida ili aweze kujikita zaidi katika fani yake.
Akiongea na www.eatv.tv Ndibalema
amesema kuwa ametafakari sana na kuamua kufanya maamuzzi hayo ili aweze
kujikita kwenye shughuli zake nje ya siasa na kudai barua ambayo
imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii ni kweli ameiandika yeye ili umma
uweze kutambua hilo.
"Nimekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Tanzania bara toka mwaka 2014 mpaka mwaka Machi 11, 2018 na barua ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ni ya kwangu na ni rasmi kabisa imetoka kwangu na niliituma usiku kuamkia tarehe 12 na lengo la kuandika barua ile ni kuwapa taarifa Umma pamoja na wanachama wa CHADEMA pamoja na wapenzi wa CHADEMA kwamba nimejivua nafasi yangu ambayo ni nafasi ya kitaifa na kubakia mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo yaani mtanzania wa kawaida kabisa na mwanachama wa kawaida"
Aidha Ndibalema ameweka wazi sababu kubwa yeye kufanya maamuzi hayo
"Nimetafakari sana na nimeamua kujikita katika shughuli zangu binafsi hasa zinazohusiana na taaluma yangu ya mawasiliano kwa Umma, nimesoma Masters ya Mass Communication kwa hiyo nataka nishughulike na mambo hayo sasa" alisisitiza Ndibalema

No comments: