Chid Benz auza mjengo wao Ilala
Msanii wa HipHop asiyeishiwa
na vituko kila uchao, Chid Benz amekiri kuuza nyumba yao ambayo
iliyokuwa kwenye 'apartment' za ghorofa waliyokuwa wanaishi Ilala Jijini
Dar es Salaam na kudai sio ya kwanza kuuza kwani ameshauza nyingi mpaka
kufikia sasa
Chid ametoa kauli hiyo kufatia mvutano mkali uliyobakia kidogo ampige
ripota wa kipindi cha eNewz kutoka EATV, Duwe Santana baada ya kutaka
kufahamu juu ya tetesi zilizokuwa zinazagaa kuwa rapa huyo ameuza
ghorofa walilokuwa wanashea katika 'apartement' za Ilala na kupolekea
kuishi kwa washkaji zake vichochoroni.
"Yeah mimi ndio nimeuza nyumba 'ghorofa' na siyo ya kwanza kuiuza nimeuza nyumba nyingi na sasa hivi naishi kwa Mama yangu mzazi ambapo nyumba nimejenga mimi. Hapa nina kwambia ni nyumba, nimezaliwa Ilala", amesema Chid Benz.
Mtazame hapa chini Chid Benz akitolea ufafanuzi juu ya kuuza nyumba yao ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

No comments: