Header Ads

Simba yawekwa kando, Yanga dimbani

Shirikisho la soka nchini TFF, kupitia Bodi ya ligi limesogeza mbele mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya Njombe Mji na Simba uliokuwa ufanyike jumapili hii kwenye dimba la Sabasaba mjini Njombe.



Bodi imefikia uamzi huo baada ya Simba kuomba mchezo huo uahirishwe ili waweze kujiandaa na mchezo wao wa marudiano raundi ya kwanza ya kombe la shirikisho kati ya Afrika dhidi ya Al Masry.
Simba inatarajia kusafiri kuelekea nchini Misri kwaajili ya mchezo huo utakaopigwa Machi 17 mjini Port Said huku ukiwa ni wa kufa na kupona ili kuamua nani anafuzu hatua ijayo baada ya timu hizo kutoka sare ya 2-2 jumatano Uwanja wa Taifa.
Kwa upande wa wapinzani wao ambao ni mabingwa watetezi wa ligi Yanga SC leo wanatarajiwa kushuka dimbani kucheza na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wao wa raundi ya 20.
 Yanga yenye pointi 40 nyuma ya Azam yenye alama 41 katika nafasi ya pili inatarajia kusafiri pia kuelekea nchini Botswana kwaajili ya mchezo wa marudiano wa ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers.

No comments:

Powered by Blogger.