DC aliagiza jeshi la polisi kukamata
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro, Sirieli Nchembe, ameliagiza
Jeshi la Polisi kumkamata Meneja wa Idara ya Maji wa Wilaya hiyo kwa
kusababisha ukosefu wa maji kwa siku tatu mfululizo.
Mkuu
huyo wa Wlilaya ameseme Meneja anayejulikana kwa jina la Herman Mundo,
pamoja na watumishi wa idara hiyo walisababisha uharibifu wa miundo
mbinu ya maji na kusababisha kukosekana kwa huduma ya maji safi kwa
zaidi ya siku tatu wilayani hapo.
Agizo hilo katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani, kilicholenga kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya alipokea malalamiko toka kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya akidai kumekua na mchezo kwa baadhi ya viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia sekta ya maji kwa kuingiza migogoro binafsi katika sekta hiyo hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi ikiwemo kukosekana kwa huduma ya maji

No comments: