Idris Sultan Adaiwa Kuwa Ndani Ya Penzi Jipyaa
Mchekeshaji
maarufu mtandaoni ambaye alijipatia umaarufu baada ya kushinda
mashindano ya Big brother 2014, Idris Sultan amesemekana kuwa ndani ya
penzi jipya na mtoto mkali balaa.
Idris
ambaye amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Muigizaji maarufu wa
Bongo movie Wema Sepetu aliwahi kukiri kuwa alikuwa hana mpenzi kwa muda
mrefu yaani alikuwa single.
Habari
za chini ya kapeti zilizopokelewa na gazeti la Ijumaa zimedai mrembo
huyo anajulikana kwa jina la Aya ambaye ana asili ya Tunisia na
inasemekana ni mrembo maarufu nchini humo.
Chanzo cha habari hizo kimeliambia gazeti la Ijumaa umbea huu ambapo kimezidi kufunguka;
"Nyie
muulizeni tu Idris atawaambia sasa ana kifaa kipya kutoka nje ya nchi
anaitwa Aya, Hivi karibuni alitua Bongo wakafanya matanuzi ya maana hadi
kuna picha nyingine zilisambaa wakiwa kwenye swimming pool wakiogelea
kimahaba”.
Baada ya kupata ubuyu huo gazeti la Ijumaa lilimsaka Idris ili kupata ukweli juu ya habari hiyo na Idris alifunguka:
"Aya
ni kweli namfahamu ni mtu wangu wa karibu sanaa lakini sina uhusiano
naye wa kimapenzi. Tumekutanishwa na programu ya mstaafu Raisi Jakaya
Kikwete, na yeye alikuja Bongo kwa ajili ya kikao na project na kuhusu
suala la kuogelea mimi sioni tatizo ijulikane tu ni mtu wangu wa
karibu”.

No comments: