Rais Kenyatta na Odinga wakutana....waapa kufanya kazi pamoja
Kwa
mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya uliofanyika October
2017, na kuleta mkanganyiko mkubwa wa kisiasa nchini humo, Rais Uhuru
Kenyatta na Kiongozi wa Upinzani wa NASA Raila Odinga leo March 9, 2018
wamekutana rasmi na kuzungumza.
Viongozi
hao wamekutana na kuzungumza kuhusu kuacha tofauti zao za kisiasa na
kutanguliza maslahi ya wananchi wa nchi hiyo kwanza kwa kufanya kazi
pamoja kurudisha amani.
“Maisha
yetu ya baadaye hayawezi kupimwa kwa Uchaguzi Mkuu unaofuata bali
utulifu wa nchi yetu na hali nzuri ya watu wetu, demokrasia ni mchakato
ambao, hiari ya watu inasikilizwa lakini maslahi ya taifa lazima
yatawale.” – Uhuru Kenyatta
Kwa
upande wake Raila Odinga ameeleza kuwa “tukiendelea kuwa wabinafsi na
waharibifu, hakuna kiwango chochote cha mageuzi ya kitaasisi ambacho
kitaboresha maisha yetu.”
Inaelezwa
kuwa wawili hao wamekubaliana kushirikiana katika agenda 9 mahususi, na
ipo kamati iliyoundwa itakayo husisha wajumbe wa pande zote mbili ili
kuanzisha programu ya kuwaunganisha tena wananchi ambao walitengwa na
milengo ya kisiasa katika kipindi cha uchaguzi.
No comments: