Msanii wa muziki wa kizazi
kipya ambaye ni mkongwe kwenye game na aneendelea kukimbiza, Judith
Wambura au Jaydee, ametoa sababu ya kuandika wimbo wake mpya wa
'Anaweza' ambao amemshirikisha msanii wa Jamaica Luciano.
Akizungumza
kwenye kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na East Africa
Television, Jaydee amesema vijana wengi sasa hivi wamekata tamaa na
maisha kutokana na mambo mbali mbali yanayowakabili, hivyo akaona ni
vyema iwapo atatunga kitu cha kuweza kuwafariji.
“Vijana wengi sana kwa kipindi hiki wameonakana kukata taa, na kuna
vitu vingi ambavyo wanapitia, mambo mengi yamekuwa kelee, party, fake
life, nimefikiri ni muda muafaka kuwapa moyo watu ambao wamekata tamaa
kuwaambia kuwa wanaweza”, amesema Lady Jaydee.
Kazi hiyo mpya ya Jaydee audio imetengenzwa na mpezni wake Spice huku video ikitengenzwa na Justine Campos wa Afrika Kusini.
No comments: