Wapinzani wa Taifa Stars watua Bongo
Timu ya taifa ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (The Leopards) kimetua nchini letayari kuikabili timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwenye mechi ya
kirafiki ya kalenda ya FIFA.
The
Leopards kimewasili jijini Dar es salaam kwa ndege kupitia uwanja wa
Mwalimu Julius Nyerere. Mchezo huo utapigwa Jumanne Machi 27, 2018
kwenye uwanja wa Taifa.
Kabla ya kucheza na DR Congo Taifa Stars, imecheza na Algeria Machi 22 na kukubali kichapo cha mabao 4-1 ugenini na sasa itakuwa na nafasi ya kujitetea mbele ya Wacongo hao.

DR Congo inashika nafasi ya 39 kwenye viwango vya ubora vya FIFA duniani kwa mwezi Februari wakati Tanzania ikiwa inashika nafasi ya 146 kwa mwezi Februari.
Tayari viingilio vya mchezo huo vimesha tangazwa ambapo mzunguko itakuwa ni shilingi 1,000 wakati VIP A, B na C itakuwa shilingi 5,000.

No comments: