Kanisa Katoliki na wanaharakati wandaa mgomo kupinga mauaji ya waandamanaji
Mgomo wa siku nzima unafanyika nchini Jamhuri ya
Kidmekrasia ya Congo, kulaani matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya
waandamanaji wanaomtaka rais Joseph Kabila kujiuzulu kuelekea Uchaguzi
Mkuu mwezi Desemba.
Mgomo huu
umeratibiwa na Kanisa Katoliki na muungano wa Mashirika ya kiraia nchini
humo ambayo yamekuwa yakiandaa maandamano dhidi ya rais Kabila.
Waandamanaji 15 wameuawa na mamia kujeruhiwa katika maandamano ambayo yamekuwa yakifanyika mwaka huu kwa mujibu wa takwimu za Kanisa Katoliki na Umoja wa Mataifa.
Omar Kavota rais wa Shirika la CEPADHO linalopigania uongozi bora na demokrasia, ameiambia RFI Kiswahili kuwa iwapo mgomo huo utaambatana na maandamano, maafisa wa usalama huenda wakatumia tena nguvu kuvunja yavunja na kusababisha maafisa na majeruhi.
Aidha, Kavota amesema huenda maandamano yasisaidie kumwondoa rais Kabila madarakani kama wanaharakati, wanasiasa wa upinzani na Kanisa Katoliki wanavyoshinikiza.
Rais Kabila amekuwa akiongoza nchi hiyo tangu mwaka 2001 lakini hajatangaza iwapo hatawania tena.
Serikali ya rais Kabila inalishtumu Kanisa Katoliki kwa kuwasaidia wapinzani kutaka kuingia madarakani kwa mlango wa nyuma.

No comments: