Kiama cha wababa wasiotunza watoto chafika
Na Fatuma Muna
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametangaza vita na wanaume wanaowapa ujauzito wanawake na kuwatelekeza kwa kuandaa jopo la Wanasheria watakaoanza kuchukuwa hatua za kisheria kwa wanaume hao kuanzia Aprili 09 mwaka huu kwenye ofisi yake.

Taarifa
hiyo imetolea na ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo imesema kwamba kitendo
cha Wanaume kukwepa majukumu ya malezi na matunzo kwa mtoto imepelekea
pia baadhi yao kutoa ujauzito, kutupa watoto na wengine kupeleka wajukuu
kulelewa na wazee na kusababisha mzigo kwa familia.
Aidha RC Makonda amesema kuwa wataangalia pia utaratibu wa kufanya marekebisho sheria ya gharama za matunzo ya mtoto kwakuwa ni ndogo na haiendani na hali ya sasa.
RC Makonda amesema lengo lake ni kuleta ukombozi kwa kinamama ili kuhakikisha wakihitaji fedha ya matumizi wanapatiwa na sio kupigwa, kusimangwa, kutukanwa na kudhalilishwa.
Hata hivyo Makonda amesema katika zoezi hilo lengo lake ni kuleta ukombozi kwa kinamama ili kuhakikisha wakihitaji fedha ya matumizi wanapatiwa na sio kupigwa, kusimangwa, kutukanwa na kudhalilishwa.
Pamoja na hayo Kiongozi huyo wa Mkoa wa Dar es salaam amesena kwamba ameamua kutoa muda wa mwezi mmoja ili kama kuna baba kwenye huu Mkoa huo anajijua ametelekeza mtoto na hatoi fedha za matunzo akamtafute na kuanza kutoa matunzo kwakuwa itakapofika Aprili 09 atachukuliwa hatua kali za kisheria.

No comments: