Golikipa aisaidia Azam FC kuipangua Yanga
Na Elbogast Myaluko
Klabu ya soka ya Azam FC imefanikiwa kurejea katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC kwenye mchezo ulipigwa jana usiku.

Makosa
ya mlinda mlango wa Mwadui FC Anord Masawe baada ya kushindwa kuondoa
mpira aliorejeshewa na mlinzi wake Idd Mobi, kisha akafanya uzembe
kuucheza na ndipo mshambuliaji Yahya Zayd akatumia nafasi hiyo kuandika
bao la kuongoza lililodumu hadi dakika 90.
Baada ya ushindi huo katika mchezo wa raundi ya 21 Azam FC sasa imeitoa Yanga katika nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 41 huku Yanga ikisalia na alama 40 katika nafasi ya pili ikiwa na michezo 19.
Yanga leo itashuka dimbani kucheza na Kagera Sugar ikiwa ni mchezo wake wa raundi ya 20 na ikishinda itarejea nafasi ya pili kwani itafikisha alama 43 na kuisogelea Simba yenye alama 45.

No comments: