Korea Kusini kutuma ujumbe maalumu kufanya ziara nchini Korea Kaskazini
Ikulu ya Korea Kusini imetangaza kwamba rais Moon Jae-in leo anatuma ujumbe maalumu kwenye ziara ya siku mbili nchini Korea Kaskazini.
Ikulu ya Korea Kusini imesema ujumbe huo utaongozwa na kiongozi wa ofisi ya usalama ya taifa Bw Chung Eui-yong, na kazi yake ni kufanya mazungumzo na maofisa wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini kuhusu masuala ya kuhimiza amani kwenye Peninsula ya Korea, na kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Zaidi ya hayo, watajadiliana kuhusu masuala ya kuhimiza mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na Marekani kwa ajili ya kutimiza lengo la kuondoa silaha za nyuklia katika Peninsula ya Korea, na suala la kuhimiza mawasiliano kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini.

No comments: