Header Ads

SERIKALI IMESEMA HAIJARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA BARABARA YA MTWARA MNIVATA.


Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mh Makame Mbalawa alipozungumza na Wananchi wa Kata ya Naliendele Jana Tarehe 4/3/2018 na kumtaka Mkandarasi anaejenga Barabara yiho kwa kiwango cha Lami kuharakisha ujenzi huo.
"Haturidhishwi na kasi ya Ujenzi wa barabara hii yenye Urefu wa Km 50 Kutoka Mtwara hadi Kijiji cha Mnivata kwa Thamani ya Tsh Bilioni 89.59 na ndio maana tunatembelea mara kwa mara kumsukuma Mkandarasi huyu afanye kwa kasi tunayoitaka" amesema.
Akijibu maswali ya baadhi ya Wananchi waliouliza kuhusu Swala la wenyeji kukosa Ajira ndogondogo na kupewa watu wa Mikoa mingine pamoja na kukosa miundombinu itakayosaidia maji yasituwame katika eneo moja, Waziri huyo amesema atayafanyia kazi kama Serikali.
Waziri Mbalawa aliongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh Evod Mmanda ambae nae alipata nafasi ya kuzungumza na Wananchi hao na kuwasihi waendelee kushirikiana na Mkandarasi huyo ili barabara hiyo iweze kukamilika kwa haraka.


 Hii ndio Barabara ya Uchumi inayojengwa kwa Kiwango cha Lami Mtwara_Mniva
 

No comments:

Powered by Blogger.