Magufuli kuweka jiwe la msingi ujenzi wa reli
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Magufuli tarehe 14 Machi, 2018 ataweka jiwe la
msingi katika sehemu ya pili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha
kisasa yaani “Standard Gauge” inayoanzia Morogoro hadi Makutupora Mkoani
Dodoma.
Sherehe
za uwekaji jiwe la msingi zitafanyika kesho kuanzia saa 3:00 asubuhi
katika kijiji cha Ihumwa nje kidogo ya Mji wa Dodoma na kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali na wananchi wa Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli hapa nchini Bw. Masanja Kadogosa anasema maandalizi ya uwekaji jiwe la msingi katika sherehe hizo yamekamilika na amewataka wananchi kujitokeza katika sherehe na waliombali na Dodoma kufuatilia matangazo yatakayorushwa hewani na vituo vya redio na televisheni
Hii ni sehemu ya pili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) kati ya awamu tano zilizopangwa kukamilisha ujenzi wa reli hiyo itakayoanzia Dar es Salaam hadi Mwanza.

No comments: