Mbowe aweka wazi jambo jema katika bajeti
Mbunge wa Jimbo la Hai na
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amefunguka na
kusema kuwa katika bajeti ya mwaka 2018/2019 serikali haijaongeza sana
matumizi ukifananisha na bajeti ya 2017/2018.
"Jambo moja ambalo nafikiri ni jema kwenye bajeti hii serikali haikuongeza sana matumizi utaweza kuona kwamba imeongeza matumizi kutoka kwenye bajeti ya mwaka jana kutoka bilioni 740 tu tofauti na mwaka jana ambapo waliongeza bajeti kwa zaidi ya trilioni tano, hata katika kinachoitwa mipango ya miradi ya kielelezo bado kilimo hakipo katika miradi ya kielelezo na kilimo kinawahudumia wananchi wengi zaidi" alisema Mbowe
Bunge la bajeti 2018/19 linatarajiwa kuanza vikao vyake Aprili 3, mwaka huu mjini Dodoma

No comments: