Marekani Yazungumzia Vitisho vya Urusi .......Ni Baada ya Putin Kutangaza Kombora Jipya Linaloweza Kutua Popote
Marekani
imepuuzia mbali mtiririko wa madai yaliotolewa na Rais wa Urusi
Vladimir Putin kuwa ana mkusanyiko wa mkakati wa silaha mpya za nyuklia
ambazo zinaweza kupiga eneo lolote duniani.
Ikulu
ya White House na Wizara ya Ulinzi zimetupilia mbali Alhamisi kauli
hizo na kuziita ni za kisiasa, wakisema jaribio la Russia kuboresha
nguvu zake za nyuklia limekuja bila kushangaza na haliwezi kuibabaisha
Marekani.
“Rais
Putin amethibitisha kile ambacho Marekani imekuwa ikikijua kwa muda
mrefu,” msemaji wa ikulu ya White House Sarah Huckabee Sanders amesema.
Russia
imekuwa ikitengeneza mifumo yenye kusudio la kudhoofisha silaha kwa
zaidi ya muongo mmoja ikikiuka moja kwa moja majukumu yake yaliyoko
katika makubaliano.
“Marekani
inaendelea kuboresha vichwa vya silaha za nyuklia viwe vya kisasa zaidi
na kuhakikisha kuwa uwezo wetu haulingani na yoyote,” ameongeza,
akigusia bajeti mpya ya dola bilioni 700 ya jeshi la Marekani.
Maafisa wa ulinzi wa Marekani pia wamesema madai ya Russia sio mageni kabisa kwao.
“Tumekuwa
tukifuatilia hatua za Russia,” msemaji mkuu wa Wizara ya Ulinzi Dana
White amewaambia waandishi Alhamisi. Silaha hizi ambazo Putin
anazizungumzia zimekuwa zikitengenezwa kwa muda mrefu sasa.”
“Wananchi wa Marekani watulie hali wakiwa na uhakika kuwa sisi tumejitayarisha kikamilifu,” amesema.
Rais
wa Urusi Vladimir Putin Alhmisi alisema jeshi lake limejaribisha silaha
kadhaa mpya za nyuklia ikiwemo aina ya kombora ambalo halina ukomo wa
masafa na linaweza kupenya ngome ya mfumo wowote unaokabiliana na
makombora.
Alikuwa
akizungumza na wabunge katika hotuba yake ya taifa kabla ya uchaguzi
mkuu kufanyika Machi 18 nchini Russia. Putin atakuwa anatumikia awamu ya
tatu kama rais na anatarajiwa kushinda na kuendelea kushikilia wadhifa
wake kwa miaka sita.
Pamoja
na kombora hilo, Putin amesema kuwa Urusi tayari imejaribisha kombora
lake jipya ambalo linauwezo wa kufika katika mabara tofauti – linaloitwa
Sarmat- ambalo ni la masafa marefu na lenye kubeba silaha nyingi zaidi
kuliko lile la awali.

No comments: