MBEGU ZA MUHOGO KUJADILIWA KWA MAENDELEO YA WILAYA - MTWARA
by Karim Faida
Ni warsha ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kujadili Masuala yahusuyo Mbegu bora za Muhogo zinazofaa kupandwa na Wakulima ili kupata mazao bora na kwa uwingi zaidi.

Katika Majadiliano hayo, Wataalam wamewataka Wakulima wa Mtwara kupanda
mbegu ya Kisasa ya Muhogo ili kuongeza kipato baada ya kuuza Mazao hayo.
Ila changamoto kubwa iliyojitokeza ni swala la Masoko ya Zao hilo la
Muhogo na Madiwani hao wameiomba Serikali kuwatafutia Masoko ya uhakika
ili kuinua kipato cha Wakulima hao.
Hata hivyo Mtaalam kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo IITA amesema Nchi ya China inahitaji Muhogo kwa wingi kutoka Tanzania kwa ajili ya utengenezaji wa vitu mbalimbali na kutoa msisitizo kwa Wakulima kulima zao hilo.
Warsha hiyo pia ilihudhuliwa na Madiwani wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Wataalam wa Kilimo akiwamo Bi Benadetha Kimata, Mtaalam wa mazao ya Mizizi na Viazi kutoka Taasisi ya Utafiti Naliendele, Devis Fabian Mwakanyamale kutoka Taasisi ya Kimataifa ya utafiti wa Kilimo (IITA) Dar_es_salaam, Efenea Komba, Afisa Kilimo Msaidizi wa Halmashauri, Joseph Tesha, Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika Wilaya pamoja na Mheshimiwa Hawa Abderehemani Ghasia, Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini ambae alikuja kama Diwani.
Akiongea na Jamii Fm Radio, Bibi Hawa Ghasia amesema hana wasiwasi na Wakulima wa Mtwara, ila kikubwa ni kupata uhakika wa Soko tu.

No comments: