Header Ads

BIASHARA KATI YA INDIA NA MTWARA KUENDELEA KUIMARIKA:


Ushirikiano wa Kibiashara kati ya Tanzania na India umeendelea kuimarika kutokana na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa zinazouzwa na kununuliwa baina ya nchi hizo mbili. Hayo yalisenwa na Mheshimiwa Sandeep Arya, Balozi wa India nchini Tanzania wakati wa Kongamano la Kukuza Biashara kati ya India na Mtwara lililofanyika jana Jumamosi tarehe 3 Machi, 2018 katika Ukumbi wa NAF Hotel Apartment, Mjini Mtwara.

Balozi Sandeep alisema asilimia 24 ya mauzo ya bidhaa za Tanzania nchi za nje kwa mwaka 2017 ziliuzwa nchini India. Mwaka 2017 Tanzania iliuza nchini India bidhaa zenye thamani ya Dola za Kimarekani 977.5 ambapo ilinunua bidhaa mbalimbali kutoka nchini India zenye thamani ya Dola za Kimarekani 1,165. Alisema mauzo ya bidhaa za Tanzania zilizouzwa India mwaka 2017 yaliongezeka kwa wastani wa asilimia 38 ikinganishwa na mauzo ya mwaka 2016
Hii ilitokana na ongezeko la bidhaa zilizozalishwa nchini ambazo zilihitajika kwa wingi huko India zikiwemo dhahabu, korosho n.k. Aidha, Balozi huyo alisema ili kuimarisha buashara kati ya Tanzania na India, serikali ya India imeondoa tozo za ushuru kwa baadhi ya bidhaa zinazosafirishwa kutoka Tanzania kwenda India zikiwemo korosho, mchele n.k na pia imefuta gharama za kibali cha kuingia India (Visa) kwa wafanyabiashara kutoka Tanzania na kubaki 7,000 tu.
Kongamano hilo liliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Mtwara na Ubalozi wa India nchini Tanzania.

No comments:

Powered by Blogger.