MBEYA CITY YAIBAMIZA MBAO FC 2-0 SOKOINE, SINGIDA UNITED CHUPUCHUPU KUPAPASWA
TIMU
ya Mbao FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC katika
mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa
Sokoine mjini Mbeya.
Ushindi huo unaifanya Mbeya City ifikishe pointi 24 baada ya kucheza mechi 21 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya saba, wakati Mbao FC inabaki nafasi ya 12 katika Ligi Kuu ya timu 16, kwa pointi zake 19 za mechi 21 pia.
Mabao ya Mbeya City mchezo wa leo yamefungwa na beki wake hodari, John Kabanda dakika ya 28 na mshambuliaji Eliud Ambokike dakika ya 47, ambaye hilo linakuwa bao lake la tisa msimu huu.
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Singida United imelazimishwa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Namfua mjini Singida.
Ruvu Shooting walitangulia kwa bao la Issa Kanduru dakika ya tisa, kabla ya beki Kennedy Wilson kuisawazishia Singida dakika ya 73.

No comments: