Mbowe na Viongozi Wengine wa CHADEMA Wafikishwa Tena Mahakamani
Viongozi
sita wa Chadema wamefikishwa leo saa 2 asubuhi katika Mahakama ya
Kisutu kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa dhamana yao, huku ulinzi
ukiimarishwa katika eneo hilo.
Kesi
hiyo inatajwa leo Machi 29, ambapo Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard, Mashauri
atatoa uamuzi kama washtakiwa hao watapata dhamana au hawatapata.
Wakati viongozi hao wakifikishwa mahakamani, Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi kuzunguka viunga vya mahakama ya Kisutu.
Katika
lango kuu la kuingia mahakamani hapo, polisi waliovalia kiraia
walifanya ukaguzi kwa kila anayeingia na kutoka na kuwazuia baadhi.
No comments: