China yasema Korea Kaskazini Imekubali kuondoa silaha za nyuklia
China
imesema kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amethibitisha katika
ziara yake ya siri huko Beijing kuwa yuko tayari kuondosha silaha za
nyuklia katika rasi ya Korea na kushiriki katika mazungumzo yatakayo
zishirikisha Korea Kusini na Marekani.
Shirika
la habari la China Xinhua, lililoweka picha za kiongozi wa Korea
Kaskazini akiwa na Rais wa China Xi Jinping, limeripoti kuwa Kim na
mkewe Ri Sol Ju walifanya ziara ya kiserikali Beijing kuanzia Jumapili
hadi Jumatano, na alihudhuria karamu maalum katika ukumbi wa Great Hall
of the People akiwa na Xi na mkewe Peng Liyuan.
Wakati
wa mkutano wao viongozi hao wawili walisisitiza umuhimu wa kuendeleza
umoja wa karibu kati ya China-Korea Kaskazini ambao ulikuwa umeingiliwa
na mvutano juu ya Pyongyang kukaidi na kuendeleza jaribio la silaha za
nyuklia na makombora ya balistika.
Xi
alikuwa amewafiki vikwazo vizito vilivyokuwa vimewekwa chini ya
usimamizi wa Marekani ili kumshinikiza Kim kurejea tena katika
mazungumzo na kuacha kutumia vitisho vya programu yake ya nyuklia ikiwa
ni suluhisho la kumaliza vikwazo vya kiuchumi, kuongeza misaada na
kuwahakikishia usalama wao.
Katika
miezi michache iliyopita, Kim alibadilisha msimamo wake wa kukataa
mazungumzo alipotangaza Korea Kaskazini ni taifa lenye silaha za
nyuklia.
Baadae
alibadilisha msimamo huo na kupunguza mvutano kwa kusimamisha majaribio
ya nyuklia na makombora, kuiacha nchi yake kushiriki katika michezo ya
Olympic huko Korea Kusini na kuwa tayari kufanya mazungumzo ya suala la
nyuklia pamoja na Rais wa Korea Kusini Moon-Jae-in ambao umepangwa
kufanyika April, na mkutano mwengine na Rais wa Marekani Donald Trump
unaotarajiwa kufanyika May 2018.
Kim
amemwambia Xi kuwa yuko tayari kutafuta ufumbuzi wa “suala al kuondoa
nyuklia” muda wa kuwa Korea Kusini na Marekani “watakuwa tayari
kushiriki katika juhudi hizi kwa nia njema, kuweka mazingira ya amani na
utulivu, wakati akichukua hatua za kusukuma mbele mazungumzo hayo na
kufikia muwafaka ili kufikia amani,” kwa mujibu wa Xinhua.
No comments: