Mkimbizi ni mtu aliyeondoka kwake nyumbani mahali anapoishi kwa sababu ya kulazimishwa, kufukuzwa au kwa hofu ya kuteswa.

Kuna mapatano ya kimataifa yanayoratibu hali hii. Chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Hadhi ya Wakimbizi kutoka mwaka 1951, mkimbizi ni mtu ambaye (kulingana na ufafanuzi rasmi katika makala 1A ya Mkataba huu), kutokana na hofu ya kweli ya kuteswa kwa sababu ya rangi, dini, utaifa, uanachama wa kikundi fulani cha kijamii, au maoni ya kisiasa, yumo nje ya nchi yake, na ameshindwa au, kutokana na hofu hiyo, hana nia ya kutegemea ulinzi wa nchi hiyo.

Dhana ya mkimbizi ilipanuliwa na Itifaki ya 1967 ya Mkataba huo na
mikataba ya kikanda katika Afrika na Amerika ya Kilatini kuwajumuisha
watu waliokimbia vita au vurugu nyingine katika nchi zao za asili.
Wakimbizi walifafanuliwa kama kundi la kisheria katika kukabiliana na idadi kubwa ya watu waliokuwa wakikimbia kutoka Ulaya Mashariki kufuatia Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Shirika la kimataifa linaloongoza juhudi za kuwalinda wakimbizi linaitwa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR kwa lugha ya Kiingereza), na liliwahesabu wakimbizi 8,400,000 duniani mwanzoni mwa mwaka 2006. Hii ilikuwa idadi ya chini kabisa tangu mwaka 1980.
Isipokuwa wakimbizi 4600000 wa Kipalestina chini ya mamlaka ya Chombo cha Umoja wa Mataifa cha Kazi ya Wokozi kwa ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina katika eneo la Mashariki ya Karibu (UNWRA kwa lugha ya Kiingereza), ambalo ni kundi la kipekee lililopeana hadhi ya ukimbizi kwa wazawa wa wakimbizi kulingana na ufafanuzi wa hapo juu.
Kamati ya Marekani kwa ajili ya Wakimbizi na Wahamiaji duniani inakadiria jumla ya wakimbizi kuwa 62,000,000 na inakadiria kuwa kuna zaidi ya watu 34,000,000 waliohamishwa makwao kutokana na vita, ikiwemo waliohamishwa makwao bila ya kuhama nchi yao, ambao wamebaki ndani ya mipaka ya taifa.
Wakimbizi wengi ambao huhama nchi zao hutafuta ukimbizi katika nchi jirani na kwao.
"Suluhisho la kudumu" kwa idadi kubwa ya wakimbizi, kama ilivyofafanuliwa na UNHCR na serikali ni: kuwarejesha kwa hiari yao kwenye nchi zao za asili; kuwajumuisha ndani ya nchi ya ukimbizi; na kuwapa makazi katika nchi ya tatu.
Kufikia tarehe 31 Desemba 2005, nchi zilizokuwa vyanzo vikubwa vya wakimbizi zilikuwa ni Afghanistan, Iraq, Myanmar, Sudan, na Maeneo ya Kipalestina.
Nchi yenye idadi kubwa ya waliohamishwa makwao nchini mwao ni Sudan, ambapo idadi hiyo ni watu milioni 5. Kufikia mwaka wa 2006, ikiwa na wakimbizi na watu wasiokuwa na makao 800,000. Wakazi wote walipohesabika, Azerbaijan ilikuwa na idadi kuu ya watu waliofukuzwa kutoka makwao ulimwenguni kote.

No comments: