Mkuu wa Mkoa atoa wiki mbili tu
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge ametoa muda wa wiki mbili
kukamilishwa kwa mkandarasi wa mradi wa Umwagiliaji unaofadhiliwa na
Mpango wa Chakula Duniani WFP, ambao ulitarajiwa kukamilika mwaka 2017
wilayani Chamwino.
Maelekezo
hayo ameyatoa katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya
Kilimo inayotekelezwa wilayani Chamwino itakayogharimu zaidi ya shilingi
milioni 800 ambapo vijiji vitatu vinatarajia kunufaika na mradi huo.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa muda uliobaki mkandarasi huyo hana budi kupelekea mafundi wote katika eneo la mradi ili kuukamilisha kwa wakati licha ya changamot zilizokuwepo hapo awali.
"Jitahidini kuanzia leo mtakuwa mmebakisha wiki mbili tu. Yaani piga ua nataka mradi ukamilike haraka iwezekanavyo. Wewe tafuta hata mafundi wako msiangalie kwamba mtapata nini sidianeni, mafundi washirikiane na Injinia huu mradi ukamilike," Mahenge.

No comments: