Yanga yaingiwa na hofu
Klabu ya Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga imeingiwa na
hofu kuelekea mchezo wake wa kimataifa dhidi ya Township Rollers FC ya
Botswana na kudai timu hiyo sio ya kuibeza kama baadhi ya watu
wanavyofikilia.
Hayo
yameelezwa na Katibu Mkuu wa wanajangwani Charles Boniface Mkwasa leo
wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuelekea mtanange
huo unaotarajiwa kuchezwa kesho (Machi 06, 2018) katika dimba la Taifa
Jijini Dar es Salaam.
"Hii timu siyo ya kuibeza ni timu ambayo inauwezo kiuchumi, nzuri na hata ukiangalia katika 'table' utaiona inaongoza kwenye ligi ya kwao Botswana. Kiukweli hii sio timu ya kuifanyia masihara", amesema Mkwasa.
Pamoja na hayo, Mkwasa ameendelea kwa kusema "nashukuru pia kusikia wachezaji wote wale waliokuwa majeruhi asilimia kubwa wamerejea katika hali zao na wamefanya mazoezi na wenzao kwa muda mrefu sasa. Tunamtegemea mwalimu na utaratibu wake wa mchezo atawachezesha wachezaji gani. Hii ni mechi kubwa yenye ushindani na mechi ambayo mshindi anakwenda katika hatua za makundi".
Mchezo wa kwanza kati ya Yanga na Township Rollers FC unatarajiwa kuchezwa kesho majira ya saa 10:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na kati na baada ya wiki moja timu ya Yanga itaradhimika kusafiri kwenda nchini Botswana kwa ajili ya mechi ya marudiano.

No comments: