JENGO
la ofisi ya serikali ya mtaa katika eneo la Goba jijini Dar es Salaam
ambalo hutumiwa na polisi, limeangukiwa na mnara wa simu kutokana na
mvua iliyonyesha juzi usiku na kumjeruhi askari.
Mvua
hiyo ambayo ilianza majira ya jioni ikiambatana na upepo mkali,
ilisababishia mnara huo kuanguka na kumjeruhi askari ambaye alikuwa
anatoa huduma kwa wananchi katika eneo hilo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Murilo, alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kueleza kuwa eneo hilo linalotumika na askari sio jengo
lao, bali ni mali ya ofisi ya serikali ya mtaa. “Katika
hilo eneo hatuna kituo cha polisi, ila polisi wetu wanakuwa wapo mobile
kwa hiyo tukiwa kwenye majengo ya serikali ya mtaa tukiwa tunatoa
huduma ina maana ni kituo cha polisi. Hivi kituo cha polisi kinakuwa na
chumba kimoja ina maana ukipita sehemu ukaona polisi watatu hicho ni
kituo cha polisi,” alihoji Kamanda Murilo. Alifafanua
kuwa wakati jengo hilo linaangukiwa na mnara kulikuwa na askari mmoja
ambaye alikuwa anatoa huduma za kiusalama katika eneo la Goba na alipata
majeraha kadhaa na hali yake inaendelea vizuri. Alisema
askari huyo alikwenda kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) na sasa yupo nyumbani akiendelea vizuri.
Mnara wa simu wajeruhi askari
Reviewed by fadhilaradio
on
1:40 AM
Rating: 5
No comments: