“Naenda South Africa Kama Kazi, Hawezi Kunikataza Mtu”- Mama Diamond
Mama
mzazi wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandra ametoa povu
zito na kusema anaweza kwenda South Africa muda wowote akitaka kwenda
kuwaona wajukuu zake na hawezi kukatazwa na mtu.
Mapema
mwaka huu Zari the Bosslady alimpiga kibuti cha maana aliyekuwa mpenzi
wake na Baba watoto wake supastaa wa Bongo fleva Diamond siku ya
Valentine’s baada ya kuchoshwa na tabia zake za kupenda michepuko.
Baada
ya kuachana Diamond alienda South Africa kwa ajili ya maandalizi ya
Albamu yake lakini cha ajabu ni kwamba hakufika kwenye nyumba aliyonunua
aliyokuwa anaishi na Zari na watoto na Tena hakufika hata kwenda
kuwaangalia watoto wake.
Baada
ya sakata hilo kutokea habari zilianza kusikika kuwa Diamond na familia
yake na mama yake mzazi hawatakaribishwa tena kwenye nyumba ya South
Africa hasa kwa sababu wamejenga ukaribu na adui namba moja wa Zari,
Wema Sepetu.
Siku
ya jana Bi. Sandra alitoleana povu na shabiki baada ya kumuuliza
kwanini hapendi kumposti mjukuu wake wa Hamisa au anamuogopa Zari kwa
sababu hataruhusiwa tena kwenda South Africa kuwaona wajukuu wake? Basi
bwana povu la Mama Diamond lilikuwa hivi:
"South Africa naenda kama kazi kwa taarifa yako na siwezi kukatazwa na mtu yoyote”.
Zari
alishasema Kwenye Interview aliyofanya na BBC Swahili kuwa hana tatizo
na familia ya Diamond kwani muda wowote wakitaka kuona watoto wao
wanakaribishwa hata Diamond akitaka kuona wanaye.

No comments: