MTOTO WA MIAKA 16 AJINYONGA MTWARA CHANZO SIMU.
Karim Faida
Binti aitwae #Salma_Abdallah, mwenye umri wa miaka 16 aliyekuwa akiishi Mtaa wa Mbawala Chini, Kata ya #Naliendele Mkoani Mtwara amejinyonga kwa kanga na kufariki Dunia ndani ya Chumba alichokuwa akilala, Jana tar 15.03.2018
.
Binti huyo ambaye amemaliza Shule ya Msingi Mkangala Mwaka 2016, amechukua uwamuzi huo, baada ya baba mlezi aitwae #Hamisi_Hassani_Lingwenje kumkuta na simu ambayo inadaiwa alipewa na Mchumba wake aliyejulikana kwa jina Moja tu la #Daudi na baba huyo kumuamuru binti huyo aende kwa bibi yake akakae kwakuwa amekuwa na mienendo isiyopendeza.
Wakati baba ameelekea sokoni ambako anafanya shughuli zake ndogondogo kuchukua pesa ya nauli ili amkabidhi binti yake, ndipo Salma alipochukua uwamuzi huo wa kujinyonga na ameacha ujumbe mzito aliouandika kwenye karatasi yakwamba "Nampenda sana Daudi, siwezi kukaa nae mbali najua hili ni kosa kwangu lakini nawaomba Wazazi wangu mumpende sana Daudi maana akiwa kwenye matatizo, Mimi sitajisikia vizuri"
Ni miongoni mwa maneno aliyoandika Marehem Salma.
Akiongea na #Jamiifm_Radio katika eneo la tukio, Mama mzazi wa Salma (Moza Mohammedi) amesema baada ya maongezi hayo kati ya baba na Salma, yeye alielekea shambani ambapo mda mfupi baadae alipigiwa simu na jirani yake kumtaka arudi nyumbani hali iliyompa wasiwasi na alipofika nyumbani alijulishwa kuhusu kifo cha Mtoto wake.
Kamanda wa Pilisi mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na mazishi yamefanyika kijiji cha Mchicha Jana Mkoani hapa.

No comments: