Header Ads

Wakazi wa Kijiji cha #Mayaya_Mtwara wamemhamisha Mfanyabiaahara

#Jembe_la_Watanzania
Wakazi wa Kijiji cha #Mayaya_Mtwara wamemhamisha Mfanyabiaahara mmoja aitwae #Abubakari_Nimtembo na tuhuma za kishirikina kwa kutaka kumfanya msukule kijana mmoja aitwae #Mohammedi_Alawi ambae alikuwa bodaboda wake.


Mfanyabiashara huyo amehamishwa Jana tar 25.03.2018 kwa tuhuma hizo ambapo inasemekana alimshawishi kijana huyo kumeza hirizi ili awe dereva maarufu wa Bodaboda ambapo siku chache mbele kijana huyo alianza kuumwa na Sehemu yake ya Sili ilizama tumboni na kuanza kuweweseka hali iliyowachanganya wanafamilia na kumpeleka kwa waganga tofauti wa kienyeji na kubaini kuwa Huyo Boss wake ndio chanzo cha ugonjwa huo na lengo ni kumfanya msukule (Ndondocha).
Kwa upande wake Mfanyabiashara huyo, Abubakari amekataa kuhusika na tukio hilo ila amekili kutoa kiasi cha pesa cha 400,000/= ili kusaidia matibabu ya kijana huyo na mke wake ambao kwa pamoja waliteswa ili wachukuliwe na wote wako kwa Mganga wa kienyeji kwa sasa wakipata huduma.

Akiongea na #Jamiifm_Radio Kijijini hapo Siku ya tukio, Mwenyekiti wa Kijiji cha #Mayaya ndugu #Mohammedi_Yusufu_Lali amethibitisha kutokea tukio hilo na kusema kwamba hapo awali Mfanyabiashara huyo alikili kufanya tukio hilo na kusema kwa sasa yupo tayari kuwatibia wagonjwa wote wawili. Aidha Serikali haijatoa kibali cha kumuhamisha Mfanyabiashara huyo ila ni Hasira tu za Wananchi.

No comments:

Powered by Blogger.