Header Ads

Mwakyembe amuonya Nay wa Mitego tena



Waziri wa Habari Dk Mwakyembe amefunguka na kumuonya msanii Nay wa Mitego kuhusu kuwadanganya wasanii wenzake na kusema ataendelea kufanya muziki ambao amekuwa akifanya miaka yote ili hali msanii huyo sasa amekuwa mstali wa mbele kufuata sheria.
Mwakyembe amesema hayo leo Machi 29, 2018 wakati waliokutana na msanii Roma Mkatoliki na waandishi wa habari na kutoa msamaha kwa msanii huyo kufuatia adhabu yake ya kufungiwa miezi sita kutojihusisha na sanaa.
"Nay wa Mitego alivyoongea na wenzake akawa anatamba kule mimi sibadilishi kitu akawa anawadanganya wenzake, Nay wa Mitego acha tabia ya kuwadanganya wenzako wakati wewe umebadilisha kila kitu na kupeleka BASATA halafu huku anatamba kwenye mitandao kwamba sibadilishi kitu, ujanja wa namna hiyo siyo mzuri anawadanganya wenzake wamuone ngangari kumbe hakuna lolote" alisema Mwakyembe
Msanii Nay wa Mitego kupitia mtandao wake wa Instgtram aliweka wazi kuwa katika wimbo wake mpya 'Mikono juu' hajabadilisha jambo lolote na kusema yeye ataendelea kufanya muziki wake kama ambavyo watu wamekuwa wakimjua kwa kuwa muziki huo wa kuchana watu ndiyo ulimtambulisha kwa jamii.

No comments:

Powered by Blogger.