Roma apewa msamaha kwa sharti moja
Wizara ya Habari, Michezo,
Sanaa na Utamaduni imemfutia adhabu Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo Roma
Mkatoliki iliyokuwa imempatia kutokana na wimbo wake wa Kiba 100 kukosa
maadili.
Akizungumza
na vyombo vya habari leo jioni, Waziri Mwakyembe amesema kwamba imeamua
kumfungulia msanii huyo baada ya kukiri kuwa amefanya makosa na kuahidi
kwamba atakuwa balozi wa maadili.
Waziri Mwakyembe amesema kuwa msamaha wa msanii huyo utaanza mara moja pale ambapo msani huyo atakamilisha sharti la kujisajili kwenye Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) huku ikiwa hajapewa muda maalumu wa kukamilisha sharti hili.
"Sisi kama wizara tumepokea maombi ya Msanii Roma na niseme Mimi kama Waziri na kwa niaba ya Naibu Waziri tumemfutia adhabu Roma Mkatoliki lakini siku atakapokabidhiwa Cheti cha Usajii cha Basata ndo siku adhabu yake itakapokuwa imekwisha" Mwakyembe.
Ameongeeza "Hatumpangii iwe lini akiweza afanye leo jioni kesho, baada ya Pasaka mwakani ni yeye, lakini siku atakapopata Cheti ndipo ataweza kuendelea na kazi zake na tunamtakia kila la kheri".
Kwa upande wa msanii Roma yeye ametoa tamko kwa mamlaka inayosimamia kazi za sanaa iweze kutoa wimbo huo katika vyombo vyote vya habari akimaanisha kuwa hataweza kuufanyia tena marekebisho yoyote kama jinsi ambavyo ilitakiwa awali

No comments: