Mwanamke Aliyemwaga Machozi Mbele ya Rais Magufuli Afungwa Jela Miezi Mitatu
Mahakama
ya Mwanzo Usambara mkoani Tanga imemhukumu kwenda jela miezi mitatu
Swabaha Shosi ambae alishawahi kushika headlines kwa kulia mbele ya Rais
Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria February 2, 2017.
Hakimu wa Mahakama hiyo Khadija Kitogo amemtia hatiani kwa kuingia eneo lisiloruhusiwa kisheria.
Swahaba
alifikishwa Mahakamani hapo August 9, 2017 akikabiliwa na shtaka la
kuingia Chongoleani ambako hakuruhusiwi Raia kuingia.
Mahakama
ilielezwa kuwa aliingia katika eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya
ujio Rais Magufuli na Yoweri Museveni walipokwenda kuzindua mradi wa
bomba la mafuta kutoka Uganda mpaka Hoima.
Swahaba
alikana mashtaka hayo na kujitetea kuwa alikanyaga eneo wakati akiandaa
eneo kwa ajili ya kuwauzia chakula waliodhuria uzinduzi huo na kwamba
hakuwa peke yake walikuwa wengi.
Hakimu
Kitogo akitoa hukumu hiyo amesema baada ya kusikiliza ushahidi wa pande
zote mahakama imemkuta na hatia ya kuvunja sheria ya Makosa ya jinai.
“Ninampa adhabu ya kwenda jela miezi mitatu ili iwe fundisho kwa wengine wanaovunja sheria kwa kuingia maeneo yasiyoruhusiwa”
No comments: