Ole-Sendeka apingana na Sumatra
Mkuu wa Mkoa wa Njombe
Christopher Ole - Sendeka amewaruhusu madereva wa bajaji Mkoani Njombe
ambao walisimamishwa kufanya shughuli zao katika barabara kuu ya Njombe -
Songea na kuruhusu bajaji kuongezwa mpaka bajaji 100 kutoka 55 ambazo
zilikuwepo.
Aidha Madereva hao wa bajaji wamedai kuwa walipeleka katika vituo ambavyo wanadai kuwa havikuwa na maslahi kwao na kwa biashara yao na hakukuwa rafiki kimiundombinu.
Hata hivyo wamiliki wa bajaji Mjini Njombe wamesema kuwa kwa muda wa wiki moja hawajaingiza fedha yoyote na kusema serikali imefanya vyema kutoa maamuzi hayo.

No comments: