Askari JWTZ adaiwa kuua kwa kugonga
Askari wa Jeshi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ), amedaiwa kusababisha kifo baada ya kumgonga
mwendesha pikipiki huko eneo la Bububu, Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
Kamanda
wa Polisi wa mkoa huo, Hassan Nassir Ali, amesema askari huyo, Hafidh
Makame Haji (40), akiwa na gari yenye namba 5512 JWTZ O7, alimgonga
Shabani Khamis (40), dereva wa pikipiki namba Z 275 FQ na kufariki
dunia.
Amesema ajali hiyo ilitokea Machi 10, mwaka huu, eneo la Bububu majira ya saa 10:15 jioni na chanzo cha ajali hakijajulikana nakuongeza kwamba jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha ajali hiyo na endapo dereva huyo atabainika kufanya uzembe, atafikishwa mahakamani.
Pamoja na hayo amewataka madereva wa vyombo vya usafiri wakiwamo madereva wa askari wa vyombo vya ulinzi na usalama, kufuata sheria za barabarani.
“Baadhi ya askari wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa na sare za kazini wamekuwa wakivunja sheria za barabarani wakiringia vyeo vyao, ninawaomba kutekeleza sheria za nchi,” amesema Kamanda Nasir.

No comments: