Papii Kocha Amefungukia Mapenzi Yake Kwa Mwanaye
Mwanamuziki
mkongwe wa muziki wa dansi Papii Kocha aliyewahi kutamba miaka ya nyuma
na wimbo wake wa ‘Seya’ amefunguka na kusema hakuna kitu kinachompa
Faraja na ushujaa kama kumuangalia mtoto wake.
Papii
Kocha alitumikia kifungo jela kwa takribani miaka minne na katika
kipindi hiko chote alimuacha binti yake aliyemtaja kwa jina la Asha
uraiani akiwa mdogo sana.
Kwenye
mahojiano aliyofanya na gazeti la ‘Amani’ Papii Kocha amekiri kuwa kwa
kipindi chote alichokaa gerezani kwa miaka kumi na nne hakupata muda
mzuri wa kukaa na mtoto wake huyo zaidi ya alivyokuwa akienda kumsalimia
gerezani lakini kwa sasa ameona afanye kila analoweza ili mwanaye aweze
angalau kufaidi matunda na furaha aliyoikosa kwa muda mrefu.
"Unajua
sijakaa na mtoto wangu kwa Kipindi kirefu sasa na hivi sasa ndio
anafaidi matunda kutoka kwa baba yake hivyo ni lazima nifanye kazi kwa
jasho jingi ili ayafaidi matunda yangu”.
Lakini
pia Papii Kocha amewasisitizia mashabiki zake kumiminika kwa wingi
kwenye Show yao inayotarajiwa kufanyika tarehe 10 machi katika ukumbi wa
King Solomon Hall.

No comments: