Header Ads

Preety Kind: Naomba Waziri Anipunguzie Adhabu Maisha Magumu

Mwanamuziki wa Bongo fleva na Muigizaji, Preety Kind amefunguka baada ya kimya kirefu na kuiomba serikali msamaha na kumuangukia Naibu Waziri Juliana Shonza amsamehe.
 

Preety Kind aliyekuwa anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘vidudu washa’ aliomshirikisha Gigy Money alifungiwa mapema mwaka huu kwenye kufanya kazi zozote za kisanaa baada ya kutuhumiwa kuvaa nusu uchi mtandaoni na hata nyimbo yake kukosa maadili.

Waziri Juliana Shonza alitangaza kuwa Preety Kind atafungiwa kwa muda wa miezi Sita ambapo hatakiwi kujihusisha na kazi zozote za kisanaa huku pia akaunti yake ya Instagram aliyokuwa anarusha picha zake za nusu utupu kufungwa.

Ikiwa Miezi michache imepita yangu adhabu hiyo itangazwe Preety Kind ameibuka na kusema kuwa maisha kwake yamekuwa magumu kwani sanaa ndio ilikuwa njia yake pekee ya kuingiza kipato kwenye maisha yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Preety Kind amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yupo kwenye harakati za kumuandikia Waziri Juliana Shonza barua ya kuomba apunguziwe adhabu kwani Mambo yanamuendea kando.

" Nimeshaomba sana msamaha na ninaendelea kuomba ambapo kwa sasa ninaandika barua ya kuomba msamaha kwa Naibu Waziri maana maisha yangu hayaendi ni magumu”.

No comments:

Powered by Blogger.