“Sasa Nataka Kuurudisha Mziki Wa Dansi Kwenye Chati”- Christian Bella
Mwanamuziki
mashughuli wa Dansi nchini Christian Bella ‘Obama’ ameweka wazi dhamira
yake ya kutaka kuurudisha muziki wa Dansi juu kwenye chati ulipokuwepo
miaka ya nyuma.
Baada
ya muda mrefu kuweka kwa malalamiko kutoka kwa mashabiki wakidai muziki
wa Dansi umepotea, sasa Christian Bella ana mpango wa kuurudisha mziki
huu juu kwa kuacha kufanya mziki wenye ladha ya Bongo fleva na kujikita
kwenye Rhumba.
Siku
za nyuma Bella aliwahi kulalamikia muziki wa Bongo fleva na kudai ndio
uliopelekea kuua kabisa soko la muziki wa Dansi nchini kwani Bongo fleva
imeonekana kuzoa mshabiki wengi zaidi na kupelekea kuua soko la mziki
wa Dansi.
Christian Bella alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv:
"Mimi
kijana wenu kijana wa kazi nataka kurudisha muziki wa bendi mashabiki
walilalamika kuwa namix sana na Bongo fleva lakini sahivi nataka
kuwarudishia muziki wa bendi, nimetoa wimbo mpya unaitwa ‘Rudi’ ili
kurudisha mziki wa Rhumba”.
Christian
Bella amehaidi kurudisha muziki wa Dansi kwenye zile Enzi ambazo
walikuwa wanajaza shoo na mapedeshee kuwatunza stejini na kuwamwagia
mahakama usiku Kocha.
No comments: