Header Ads

Serikali ya Libya yataka kusimamisha vita katika eneo la kusini

Serikali ya Libya yataka kusimamisha vita katika eneo la kusini
Serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa inataka kusimamisha mara moja mapigano katika mji wa Sabha uliko kusini mwa nchi hiyo, ambako raia wengi wameuawa na kujeruhiwa katika mapigano ya kikabila.
Taarifa iliyotolewa na serikali ya nchi hiyo imesema, baraza la rais la serikali ya umoja wa kitaifa limeeleza kusikitishwa sana na mapigano yanayoendelea kati ya ndugu wa Libya huko Sabha, huku ikitaka pande zote kujizuia na kurejesha mazunguzo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, serikali pia inaunda kamati ya kutimiza kusimamisha mapigano na kurujesha utulivu katika eneo la kusini.

No comments:

Powered by Blogger.