NEYMAR AWASILI BELO HORIZONTE KWA AJILI YA UPASUAJI ASIKOSE KOMBE LA DUNIA
NYOTA wa Paris Saint-Germain, Neymar amewasili
mjini Belo Horizonte akiwa na mama yake, Nadine Goncalves Da Silva
and na Daktari wa timu ya taifa ya Brazil, Rodrigo Lasmar jana tayari
kwa upasuaji wa mguu.
Nyota
huyo wa anatarajiwa kufanyiwaupasuaji wa mguu baada ya kuumia enka
Jumamosi iliyopita, timu yake PSG ikishinda 3-0 katika Ligi ya Ufaransa,
Ligue 1 dhidi ya Marseille.
Pamoja
na klabu yake awali kusema mchezaji huyo hakuhitaji upasuaji, lakini
mshambuliaji huyo jana usiku aliwasili katika hospitali ya Mater Dei
Hospitalhuyo nchini kwao, Brazil.
Brazil
imeamua kumchukua Neymar kumtibu haraka ili isije ikamkosa kwenye
Fainali za kombe la Dunia nchini Urusi katikati ya mwaka.
Sasa
PSG wanaelekea kwenye mchezo wa marudiano wa 16 Bora Ligi ya Mabingwa
Ulaya wiki ijayo bila Neymar wakitakiwa kuifunga Real Madrid 2-0 mjini
Paris ili kwenda Robo Fainali, kufuatia kufungwa 3-1 kwenye mchezo wa
kwanza Madrid.

No comments: