Header Ads

Tanzania Prisons yatangaza kiama



Timu ya Tanzania Prisons yenye maskani yake mitaa ya Sinde jijini Mbeya leo imeendelea na mazoezi ya kujifua kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Jkt Tanzania, unaotarajiwa kupigwa siku ya Jumamosi (Machi 31, 2018) katika viwanja vya kumbukumbu Sokoine.
Prison ambayo imetinga hatua ya robo fainali katika michuano ya ASFC inahitaji ushindi mnono ili kujihakikishia nafasi nzuri kwenye kinyang’anyiro cha ushindi katika Ligi hiyo.
Akizungumzia maandalizi hayo Kocha wa Tanzania Prison Mohammed Abdalla amesema kikosi chake kipo imara kutokana na kufanya mazoezi ya kutosha ambayo yamedumu wiki mbili sasa.
Kwa upande wake nahodha wa Prisons Benjamin Asukile, amedai kuwa Timu ya Jkt Tanzania sio ya kubeza  kutokana na ushindani pamoja na ufundi wao uwanjani hivyo wamejipanga kuikabili.
Timu ya Tanzania Prison inashika nafasi ya nne  ikiwa na pointi 36 katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara nyuma ya Timu ya  Azam Sport Club.
Mtazame hapa chini nahodha wa Prisons Benjamin Asukile akifunguka zaidi kuelekea mchezo huo.

No comments:

Powered by Blogger.