Header Ads

Times FM Waomba Radhi kwa Kauli za Msanii Diiamond


Kituo cha Redio Times cha jijini Dar es Salaam kilichorusha mahojiano ya  mwanamuziki Diamond Platnumz kimeomba radhi kwa kauli tata zilizozua mjadala nchini.

Taarifa hiyo iliyowekwa  katika mtandao wa kijamii wa Instagram, ilisema imeamua kuomba radhi kutokana na kauli tata alizotumia msanii huyo wakati akihojiwa katika kipindi cha Play List kinachoongozwa na mtangazaji Omary Tambwe.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba siku hiyo Diamond alialikwa katika kipindi hicho  kwa ajili ya kupongezwa kwa kumpa tuzo maalumu nyota wa mchezo kwa mchango wake kwenye muziki na  kutoa ajira kwa vijana.
 

Jingine ni kutangaza lugha ya Kiswahili kupitia muziki na kupeperusha bendera ya Tanzania kupitia sanaa ya muziki na kutoa albamu yake mpya ya ‘A Boy From Tandale ‘  ambapo kituo hicho kilimtaja kama msanii bora wa kiume, msanii bora wa kimataifa kwa kuvunja rekodi na  msanii mwenye ushawishi zaidi na pia kumpatia tuzo maalum (Plaque).

“Kwa namna ambayo haikutarajiwa , mwanamuziki huyo alitumia kauli  tata dhidi ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Juliana Shonza katika mahojiano hayo.
 
“Uongozi wa Times unaomba radhi kwa Wizara, Naibu Waziri, TCRA, Basata pamoja na umma kutokana na kauli hiyo ya Diamond kwani Times haikuwa dhamira yetu kwa sintofahamu hiyo na tumekuwa tunafanya jazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za utangazaji,” imesema taarifa hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.