TRA yawatumbua wawili
Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) imewasimamisha kazi watumishi wake wawili mkoani Lindi, kwa kile
kilichodaiwa kwenda kinyume na kanuni na miongozo ya kazi
inavyowaelekeza na kutumia lugha isiyo rafiki na wateja wao
{wafanyabiashara}.
Uamuzi
huo,umechukuliwa na Kamishina kodi ya Mapato za ndani nchini, Elijah
Mwandumbya, wakati wa kikao cha pamoja kati yake na wafanyabiashara wa
mkoa huo,kilichofanyika Manispaa ya Lindi baada ya kusikiliza malalamiko
mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Mwandumbya amesema Taifa wamekuwa wakipata taarifa kwamba hakuna mahusiano mazuri kati watumishi hao na wafanyabiashara, hali iliyohustua uongozi na kumtuma Kamishina huyo kufika mkoani humo kupata maelezo ya kina.
Kamishina huyo wa kodi za ndani amesema {TRA} inapitia kipindi ambacho kinahitaji kuwapatia huduma bora wateja wao ili waweze kumsaidia Rais wa nchi katika utekelezaji wake wa maendeleo kwa kuhakikisha wanazingatia Sheria, kanuni, taratibu na miongozo,kuhakikisha wanatoa huduma iliyo bora kwa walipa kodi.

No comments: