Header Ads

Zijue Sheria za Kazi: Haki za Msingi za Mfanyakazi

Maazimio ya pamoja ya Shirika la Kazi Duniani (ILO)


  • Yanahusu zaidi kanuni za kisheria ambazo zinatoa miongozo na haki katika sehemu ya kazi
  • Kwa ufupi, miongozo na haki sehemu za haki zinahusiana na;
1. Ajira za watoto: No 138/1973; 182/1999
2. Kazi za lazima: No 29/1930;105/1951
3. Ubaguzi: No.111/1958; 100/1951
4. Uhuru wa kuungana na kuingia makubaliano ya hiari ya pamoja: No.87/1948; 98/1949

Haki za mtoto S.5
  • Inazuia ajira kwa mtoto yeyote mwenye umri chini ya miaka 14
  • Mtoto mwenye umri wa miaka 14 au zaidi anaweza kuajiriwa kufanya kazi nyepesi tu,
  • Inazuia kumfanyisha mtoto kazi nyakati za usiku.
  • Ajira zinazozuliwa hapa ni pamoja na aina mbaya za ajira za mtoto kama utumwa, usafirishaji wa watoto, uwekaji rehani kwa ajili ya deni na aina zote za ajira za shuruti, biashara ya ngono na utengenezaji filamu za ngono, kuajiri watoto kwa lazima kwa shughuli za kijeshi n.k
Tazama pia Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

Kazi za lazima S.6
Sheria inakataza kazi za lazima lakini inatoa nafasi kwa aina fulani za kazi za lazima kama;
  • Kazi yoyote inayotekelezwa chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taifa ya mwaka 1966, kwa kazi ambayo ni ya kijeshi.
  • Kazi yoyote ambayo ni sehemu ya wajibu wa kawaida wa kiraia kwa raia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Kazi yoyote inayotekelezwa kwa dharura au hali ya hatari.
  • Kazi yoyote inayotolewa kwa mtu yeyote ikiwa ni matokeo ya kutiwa hatiani na mamlaka ya sheria.
Kuzuia ubaguzi sehemu ya kazi

S.7 - (1) Kila mwajiri atatakiwa kuhakikisha kwamba anaendeleza fursa sawa katika ajira na kujitahidi kuondoa ubaguzi katika sera yoyote ya ajira mazoezi kwa vitendo

(2) Mwajiri atalazimika kusajili kwa Kamishna wa Kazi, mpango wa kuendeleza fursa sawa na kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi

(3)Kamishna wa Kazi anaweza kumtaka mwajiri:-
  • Kuunda mpango wa kuendeleza fursa sawa na kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi kama inavyoelekezwa katika kifungu kidogo cha (2); na
  • Kuusajili mpango huo kwa Kamishna
  • Kutokuunda mpango huo na kuusajili ni kosa kisheria

(4) Mwajiri yeyote asifanye ubaguzi wa dhahiri au usiokuwa wa dhahiri kwa mwajiriwa, katika sera au mazoea katika moja ya sababu zifuatazo:

a)Rangi
b)Utaifa
c)Kabila au sehemu anayotoka
d)Asili
e)Uasili wa Taifa
f)Asili ya kijamii
g)Maoni ya kisiasa au kidini
h)Mwanamke au Mwanaume
i)Jinsia
j)Ujauzito
k)Kuolewa ama kutoolewa au majukumu ya familia
l)ulemavu
m)VVU/UKIMWI
n)Umri; au
o)Maisha anayoishi

HAKI KUUNGANA WAAJIRIWA

S 9 - (1) Kila mfanyakazi ana haki ya;

a)Kuunda na kujiunga na chama cha wafanyakazi.
b)Kushiriki katika kazi halali za chama cha wafanyakazi.

S 9 - (3) Mtu yeyote haruhusiwi kufanya ubaguzi kwa mfanyakazi kwa sababu huyo:-
  • Ametekeleza au alitekeleza haki yoyote chini ya Sheria hii au Sheria nyingine inayosimamiwa na Waziri.
  • Ni mwanachama au alikuwa mwanachama wa chama cha Wafanyakazi; au
  • Ameshiriki au alishiriki katika kazi halali cha chama

S 9(4) Mtu yeyote haruhusiwi kufanya ubaguzi, kwa mfanyakazi wa chama cha wafanyakazi au shirikisho kwa kukiwakilisha au kushiriki katika kazi halali za chama.

S 9(5) Mtu yeyote anayekiuka masharti ya vifungu vidogo vya (3) na (4), anatenda kosa.

S 9(6) Kwa madhumuni ya kifungu hiki;

a)“mfanyakazi” inajumuisha mwombaji wa kazi;
b)“mfanyakazi wa ngazi ya juu ya uongozi” maana yake ni mfanyakazi ambaye, kulingana na nafasi ya mfanyakazi huyo-
  1. Anatengeneza sera kwa niaba ya mwajiri; na
  2. Anaruhusiwa kuingia mikataba ya hiari kwa niaba ya mwajiri.

HAKI YA KUUNGANA WAAJIRI


S. 10 - (1) Kila mwajiri atakuwa na haki-

a)Kuunda na kujiunga na chama cha waajiri;*
b)Kushiriki katika kazi halali za chama cha waajiri,

S .10 - (2) Mtu yeyote haruhusiwi kufanya ubaguzi kwa mwajiri kwa sababu mwajiri-
  • Ametekeleza au alitekeleza haki yoyote chini ya Sheria hii au Sheria inayosimamiwa na Waziri;
  • Ni mwanachama au alikuwa mwanachama wa chama cha waajiri; au
  • Ameshiriki au alishiriki katika kazi halali za chama cha waajiri.

VIWANGO VYA AJIRA

1. Mikataba ya Ajira

a). Aina za mikataba
  1. Mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa (mara nyingi huitwa mkataba wa kudumu)
  2. Mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa
  3. Mkataba wa kazi maalumu
Kazi maalumu - maana yake ni zile zinazotokea mara chache au za msimu ambazo sio endelevu. ( ELRA Misc. Amendment No 38 of 2015; S.4)

b). Taarifa ya maelezo ya maandishi S.15
15-(1) Mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi, maelezo ya mkataba kwa maandishi kama-

i. Jina, umri, anuani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi
ii. Mahali alipoajiriwa
iii. Kazi yake
iv. Tarehe ya kuanza
v. Muundo na muda wa mkataba
vi. Kituo cha kazi
vii. Masaa ya kazi
viii. Ujira, njia ya ukokotoaji wake, na taarifa za mafao mengine au malipo ya vitu; na
ix. Kitu kingine kilichotajwa

(2) Kama taarifa zote zilizotajwa katika kifungu kidogo cha (1) zimeelezwa kwenye mkataba wa maandishi na mwajiri amempa mfanyakazi mkataba huo, mwajiri anaweza asitie maelezo yaliyoandikwa yaliyotajwa katika kifungu cha 14.

(3) Kama mfanyakazi haelewi maelezo yaliyoandikwa , mwajiri anatakiwa kuhakikisha kwa yanafafanuliwa kwa mfanyakazi katika hali ambayo mfanyakazi anaelewa.

(4) Pale ambapo suala lililotajwa katika kifungu kidogo cha (1) litabadilika, mwajiri atatakiwa kwa kuwasiliana na mfanyakazi, kurekebisha maelezo yaliyoandikwa ili kuendana na mabadiliko na kumtaarifu mfanyakazi mabadiliko hayo kwa maandishi.

(5) Mwajiri atatakiwa kutunza maelezo ya maandishi yaliyotajwa katika kifungu kidogo cha (1) kwa muda wa miaka mitano baada ya kusitishwa kwa ajira

(6) Ikiwa katika mwenendo wowote wa kisheria, mwajiri atashindwa kutoa mkataba wa maandishi au maelezo ya maandishi yaliyotolewa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1), jukumu la kuthibitisha au kukanusha sharti la ajira linalodaiwa na lililotajwa katika kifungu kidogo cha (1) litakuwa ni la mwajiri.

(7) Masharti ya kifungu hiki hayatatumika kwa mfanyakazi ambaye anafanya kazi chini ya siku sita kwa mwezi kwa mwajiri.

2. Masaa ya Kazi

a) Masaa ya kazi – Masaa 9 kwa siku; Masaa 45 kwa wiki; na Siku 6 katika wiki yoyote

b) Si zaidi ya saa 50 ya ziada katika mzunguko wa wiki nne

c) Mwajiriwa hatatakiwa kufanya kazi zaidi ya masaa 12 kwa siku hata kama wamekubaliana hivyo (kifungu cha 19)

d) Kazi zitakazofanyika usiku kati ya saa 02:00 usiku na saa 12.00 asubuhi, Mwajiri atatakiwa kumlipa mfanyakazi angalau 5% ya mshahara wa mfanyakazi huyo kwa kila saa atakayofanya kazi usiku na kama saa anayofanya kazi ni ya ziada; 5% itakokotolewa katika kima cha saa za zaida za mfanyakazi. (Kifungu cha 20(4)).

NB:
Kazi za usiku haziruhusiwi kwa mwanamke mjamzito miezi miwili kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua, au miezi miwili baada ya tarehe ya kuzaa . (Kifungu 20(2))

e) Mapumziko katika siku ya kazi
S.23 - (1): Mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi ambaye amefanya kazi mfululizo kwa zaidi ya saa 5 mapumziko ya angalau dakika 60. (Break given if the job can be left unattended)

(2) Mwajiri anaweza kumtaka mfanyakazi kufanya kazi wakati wa mapumziko ikiwa tu kama kazi haiwezi kufanywa na mfanyakazi mwingine.

(3) Mwajiri hatakiwi kuwajibika kumlipa mfanyakazi katika kipindi cha mapumziko isipokuwa kama mfanyakazi anatakiwa kufanya kazi au kuwepo kwa ajili ya kazi wakati wa mapumziko


3. Ujira
a) S.26 (2): Kima cha ujira kwa saa, siku au mwezi kitatakiwa kuamuliwa kwa kufuata orodha iliyotolewa katika Jedwali la Kwanza

b). Malipo ya fedha yatakuwa katika bahasha iliyofungwa kama malipo yanafanyika kwa fedha taslimu au kwa hundi (Kifungu 27 (1)(c)); au fedha iwekwe katika akaunti ya benki ambayo mfanyakazi ameichagia mwenyewe kwa maandishi.

c). Mwajiri hatakiwi kufanya makato yoyote kwenye ujira wa mfanyakazi isipokuwa tu yale ambayo yapo kwa mujibu wa Sheria ama mfanyakazi amekubali kukatwa kuhusiana na deni.

d). Malipo yafanyike katika muda wa kazi, mahali pa kazi katika siku waliyokubaliana.


4. Likizo ya mwaka

a). Anayestahili:
Mfanyakazi mwenye miezi chini ya sita kazini hatakuwa na haki ya kupata likizo yenye malipo chini ya masharti ya sehemu hii. ELRA, see Section 29 (1)

Mfanyakazi mwenye utumishi wa chini ya miezi sita na ambaye amefanya kazi zaidi ya mara moja katika mwaka, atakuwa na haki ya kupata likizo yenye malipo chini ya masharti ya Sehemu hii kama jumla ya kipindhi alichofanya kazi kwa mwajiri huyo kinazidi miezi sita kwa mwaka huo. S.29-(1) (b)

S.30-(1) (c) “Likizo yenye malipo” maana yake ni likizo yoyote inayolipwa chini ya Sehemu hii na inayokokotolewa kwa kuangalia mshahara wa kawaida wa mfanyakazi.

S.31-(1) Likizo ya Mwaka; Mwajiri atatakiwa kutoa kwa mfanyakazia angalau siku 28 mfululizo kuhusiana na kila mzunguko wa likizo, na likizo hiyo itajumuisha siku yoyote ya sikukuu ambayo inaweza kuangukia ndani ya kipindi cha likizo

Employment and Labour Laws (Miscellaneous Amendment 2015- amends sect 31 on LEAVE

(6) Kwa makubaliano na Mfanyakazi, Mwajiri anaweza kumruhusu Mwajiriwa kumfanyia kazi katika kipindi ambacho Mfanyakazi huyo alitakiwa kuwa likizo kwa sharti kwamba mwajiriwa huyo asifanye kazi mfululizo kwa miaka miwili. (yaani unamuuzia mwajiri wako likizo yako)

(7) Mwajiri atamlipa mfanyakazi mshahara wa mwezi mmoja badala ya likizo ya mwaka ambayo mfanyakazi alitakiwa kwenda ama alitakiwa na mwajiri kumfanyia kazi badala ya kwenda likizo hiyo.


5. Likizo ya Ugonjwa (Kifungu cha 32

• siku 63 za kwanza – mshahara mzima
• siku 63 zinazofuata – nusu mshahara

Jumla ya siku 126 ambazo mfanyakazi atakuwa na haki ya likizo ya ugonjwa katika kila mzunguko wa likizo (Mzunguko wa likizo katika Sehemu hii ni miezi 36)

ED zinahesabika kama sehemu ya likizo ya ugonjwa

Likizo itatolewa kwa mfanyakazi kuwasilisha kwa mwajiri cheti cha matibabu kilichotolewa na tabibu aliyesajiliwa au tabibu mwingine yeyote anayekubalika na mwajiri, ambacho kukubalika kwake hakutakiwi kukataliwa bila sababu za msingi.

6. Likizo ya uzazi

i). Taarifa (S.33(1)) Mfanyakazi mwanamke atoe notisi kwa mwajiri kuhusiana na kusudio lake la kuchukua likizo ya uzazi angalau miezi mitatu kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua na notisi hiyo italazimika kuambatana na cheti cha kitabibu.

ii). Mfanyakazi anaweza kuanza likizo ya uzazi muda wowote kutoka wiki nne kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua, au tarehe ya mapema kama tabibu atathibitisha kwamba ni muhimu kwa afya ya mfanyakazi au ya mtoto wake ambaye hajazaliwa

iii). Mfanyakazi hatatakiwa kufanya kazi ndani ya wiki sita baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake, labda tabibu awe amethibitisha kuwa anaweza kufanya hivyo. (Section 33(3)

iv). Likizo ya uzazi itakuwa siku 84 au siku 100 kama mfanyakazi atajifungua watoto zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. (Section 33 (6)

v). Mfanyakazi mjamzito au anayenyonyesha hataruhusiwa kufanya kazi ambazo ni hatari kwa afya yake au kwa afya ya mtoto wake., mwajiri atalazimika kumpa kazi nyingine mbadala inayofaa ikiwa inawezekana, kwa masharti na mazingira ambayo si mabaya zaidi ya masharti na mazingira yake.

vi). Mfanyakazi atakuwa na haki ya masaa hadi mawili kwa siku ya kumnyonyesha mtoto wakati wa saa za kazi.

(G.N No.47 Employment and Labour Relations (General) Regulations, 201)
"Mfanyakazi mwanamke, kwa kipindi kisichopungua miezi sita mfululizo baada ya kuisha kwa likizo ya uzazi, atatakiwa kuondoka mahali pa kazi angalau kwa masaa mawili katika wakati anaoona unafaa, kwa ajili ya kunyonyesha mtoto"

7. Likizo ya Uzazi ya baba na aina nyingine za likizo

a). Angalau siku 3 za likizo ya uzazi ya baba yenye malipo kama:
  • Likizo itachukuliwa ndani ya siku 7 tangu kuzaliwa mtoto
  • Mfanyakazi ni baba wa mtoto. (Section 34 (1)(b) and 34(1)(b)).
b)Angalau siku 4 za likizo ya malipo kwa sababu zifuatazo
  • Ugonjwa au kifo cha mtoto wa mfanyakazi
  • Kifo cha mke wa mfanyakazi, wazazi, bibi na babu, mjukuu au kitukuu
Siku 3 zilizotajwa hapo juu ni jumla ya idadi ya siku ambazo mfanyakazi ana haki bila kujali watoto wangapi wa mfanyakazi wamezaliwa ndani ya mzunguko wa likizo

No comments:

Powered by Blogger.