Uganda yasaini mkataba na Kenya
Serikali ya Uganda imesaini
makubaliano na nchi jirani ya Kenya ya kuiuzia tani laki sita za mahindi
kila mwaka, hatua ambayo inatoa uhakika wa soko kwa wakulima wa mahindi
wa Uganda ambao kwa miaka mingi wamehangaika kuuza mahindi ya ziada.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza la Nafaka la Uganda, Chris Kaijuka, bado
shehena kubwa ya mahindi inasafirishwa kwenda katika nchi mbalimbali
bila kibali maalum ikiwemo Rwanda, Sudan na Kenya.
Imebainika kuwa Uganda huzalisha takriban tani milioni nne za mahindi kwa mwaka, ambapo kiasi kidogo sana hutumika nchini humo huku 80% yakisafirishwa kama nafaka kwenda kwenye masoko ya Kikanda.
Mmoja wa wasafirishaji wa mahindi kutoka Uganda, Haji Abudalla Kamira, amesema chini ya makubaliano hayo sasa tani moja ya mahindi itauzwa kwa dola za Kimarekani 225 katika soko la Kenya

No comments: