Waziri Mwijage akiri kuchukizwa
Waziri wa Viwanda, Biashara
na uwekezaji Charles Mwijage amesema kuwa hapendezwi na bei elekezi za
sukari zilizopo kwa sasa na anajitahidi kutengeneza viwanda vidogo vya
sukari kama 100 ili soko la sukari lijiendeshe lenyewe.
Amesema
hayo katika ziara yake ya kushtukiza mkoani Manyara na kuweza
kutembelea kiwanda kidogo cha sukari cha Manyara Sugar na kuona
uzalishaji uliopo na kusema kuwa kupanda kwa bei nikutokana na viwanda
vingi kufungwa lakini serikali imetoa vibali vya kuagiza tani mia moja
thelathini elfu na kwa sasa zimeshaanza kuingia na mpaka mwezi wa sita
zitazuiliwa ikiwa tayari viwanda vya ndani vitaanza kusambaza sukari
hiyo.
Pamoja na hayo Waziri Mwijage amefungua eneo maalumu la ujenzi wa viwanda ambalo linaukubwa wa ekari 9.14 ambapo ekari 6.855 litajengwa majengo matatu ambayo yataanzishwa viwanda kumi vidogo.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Manyara Sugar BW. Bharabat Sesodya amesema kuwa kutotosheleza kwa sukari ni kutokana na udogo wa uzalishaji lakini kwa sababu mwaka huu wanamiwa ya kutosha lazima wafikie lile lengo la serikali lililo kusudia.

No comments: